
Mabingwa wa Afrika wamefuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika kwa bahati, baada ya kuzidiwa nguvu katika dakika 90 za mchezo.
Uganda ndio waliowafanya Zambia wakeshe wakiomba, baada ya kuwatungua kwa bao moja jijini Kampala.
Hiyo ilikuwa kulipiza kisasi kwa Zambia waliowachapa bao hilo hilo mjini Ndola, Zambia mwezi uliopita.
Timu ya kufuzu kushiriki mashindano hayo yatakayofanyika Afrika
Kusini hakuweza kupatikana, hata baada ya Zambia na Uganda kupigiana
penati tano tano, kwani walikuwa nguvu sawa.
ilibidi mikwaju zaidi ya penati iongezwe hadi mshindi apatikane,
ndipo ikabidi mabingwa waende hadi penati ya 10 ili kupata ushindi, na
sasa wana kazi kubwa ya kutetea kombe.
Wa Zambia ulikuwa ushindi wa penati 9-8, ambapo Patrick Ochan wa
Uganda alikosa penati muhimu, katikati ya kelele za washabiki wa Uganda
waliotaka kuona timu yao ikiingia kwenye fainali hizo.
Mechi hiyo ilijenga ushindani wa aina yake uliokaribia na uhasama,
ambapo Uganda kwa mara nyingine wamekosa nafasi ya kufuzu kwa asilimia
ndogo kabisa.
Kwa mpira ulivyoanza Jumamosi hii jijini Kampala, wakiwa na
uungwaji mkono wa maelfu ya washabiki wao, Uganda walionekana kuwa na
nafasi nzuri ya ushindi.
Na kweli, katika dakika ya 27 tu mambo yalijipa, kwani Geoffrey
Massa aliandika bao la kuongoza, huku Uganda wakiwachezesha Zambia kwata
na kuwafanya wahemee juu juu.
Uganda waliendelea kucheza kwa kujituma ili kutafuta bao la pili
ambalo lingewahakikishia kufuzu moja kwa moja, lakini kikosi hicho
kinachonolewa na Mskochi, Bobby Williamason kilishindwa kuwazidi nguvu
mabingwa.
Golikipa wa Zambia, Kennedy Mweene atakumbukwa na Waganda, kwani
alizuia nafasi zao za wazi za kuandika mabao, kushinda na kufuzu,
kutokana na jinsi alivyocheza kwa ushujaa.
Nyota ilionekana kulalia kwa wenyeji bado, kwani wageni walipoanza
kupiga penati, walikosa ya kwanza kupitia kwa nahodha wao, Chris
Katongo.
itakumbukwa kwamba, Katongo ndiye alikuwa chachu ya ushindi
uliowafanya Zambia kutawazwa mabingwa wa Afrika, hivyo alipewa nafasi ya
kwanza akiaminika angefunga, ili awatie nguvu wenzake, lakini haikuwa
hivyo.
Hata hivyo, Uganda walishindwa kutumia fursa hiyo kwa uendelevu,
nao wakafikia mahali wakashindwa, hadi ilipofika fursa ya Ochan
aliyeshindwa kufanya kweli.
Zambia walishinda mechi ya fainali ya kombe hilo mwaka huu kwa
mikwaju ya penati dhidi ya Ivory Coast, katika fainali zilizofanyika
Libreville, Gabon.
walihamasika kucheza vyema, maana fainali hizo zilifanyika karibu
na ufukwe ambao wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia walifia
kwa ajali ya ndege mwaka 1993.
Uganda ilikosa ushiriki wa fainali zilizopita kwa ncha ya sindano,
walipokwama kushinda mechi ya mwisho ya kufuzu iliyofanyika Kampala.
mara ya mwisho kushiriki fainali hizo ni 1978, ambapo walifika hadi fainali, wakaishia kuwa washindi wa pili.
Timu ya taifa ya Mali iliichapa Botswana mabao 4-1 na kujikatia
tiketi ya kushiriki fainali hizo, katika mchezo uliofanyika kwenye
uwanja uliokarabatiwa wa Lobatse.
Magoli ya Mali yalifungwa na Cheikh Tidiane Diabate, Modibo Maiga,
Mahamadou Samassa na Abdou Traore na kuwafanya Mali wawe na ushindi wa
jumla wa mabao 7-1.
Mali walishika nafasi ya tatu kwenye fainali zilizopita.
Ghana walikuwa wa kwanza kufuzu kwa fainali hizo, baada ya mchezaji
wao mahiri, Afriyie Acquah kufunga bao pekee kwenye mchezo wake dhidi
ya Malawi uliofanyika mjini Lilongwe.
Acquah aliitwa kwenye kikosi hicho dakika za mwisho kuchukua nafasi
ya majeruhi. Katika mchezo wa kwanza, Ghana walishinda mabao 2-0
nyumbani.
Timu hiyo ya Afrika Magharibi ilikuwa ikipewa nafasi kubwa kutwaa
kombe mwaka huu, lakini waliishia nusu fainali, walipotolewa na Zambia.
Waliishia kushika nafasi ya nne, baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Mali katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.
fainali za Mataifa ya Afrika zinafanyika nchini Afrika Kusini
kuanzia Januari 19 hadi Februari 10 mwakani, na ni moja ya michezo yenye
mvuto barani Afrika na kwingineko.
No comments:
Post a Comment