13 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI TWFA

Wagombea 13 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA)
wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika juzi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni
Zavala, waliopitishwa kwenye nafasi ya uenyekiti ni Isabellah Huseein
Kapera, Joan Ndaambuyo Minja na Lina Paul Kessy.
Makamu Mwenyekiti ni Rose Kisiwa wakati wanaowania nafasi ya Katibu
Mkuu ni Amina Ali Karuma na Cecilia Oreste Makafu. Mgombea pekee wa
nafasi ya Katibu Msaidizi, Macky Righton Mhango naye amepita kwenye
usaili huo. Aliyepitishwa kwenye nafasi ya Mhazini ni Rose Stewart
Msamila.
Furaha Francis na Zena Chande wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati
waliopita kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia
Ludovick Temba, Rahim Salum Maguza na Sophia James Charles.
Hivi mchakato wa uchaguzi wa TWFA uko katika kipindi cha kukata
rufani ambapo ni kuanzia Oktoba 15-17 mwaka huu. Rufani zinatakiwa
zifike kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Oktoba 17
mwaka huu.
Wagombea wawili ambao hawakupitishwa kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka huu ni Julliet Mndeme na
Jasmin Soud walioomba ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF. Wagombea hao ambao
pia walikuwa wamewekewa pingamizi hawakufika kwenye usaili.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA ARFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa
uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA)
uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 14 mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho
unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA walivyo na imani kubwa
kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Pwani.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya
COREFA chini ya uenyekiti wa Hassan Othman Hassan ambaye amechaguliwa
tena kuongoza chama hicho.
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha
unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Pwani kwa kuzingatia katiba
ya COREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa
kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Hassan Othman Hassan
(Mwenyekiti), Riziki Majala (Katibu), Geofrey Irick Nyange (Mjumbe wa
Mkutano Mkuu TFF), Juma Haruna Kisoma (Mwakilishi wa Klabu TFF) na
Abubakar Allawi (Mhazini).
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi
huo uliofanyika kisiwani Mafia ni Musa Bakari Athumani, Godfrey Magnus
Haule na Gwamaka Oden Mlagila. Mwakilishi wa Wanawake ni Florence
Ambonisye.
No comments:
Post a Comment