Wednesday, October 24, 2012

Messi, Xavi and Iniesta, World Soccer award finalists

The three Blaugranas are among the finalists for the best player of the year award given out by World Soccer magazine

 Messi current holder of the World Soccer award. PHOTO FCB.

 Three FC Barcelona players are among the ten candidates for the best player of the year award given out by World Soccer. Leo Messi, Xavi Hernández and Anrdés Iniesta will compete for the prize with Touré Yaya (Manchester City), Didier Drogba (Shangai Shenhua), Eden Hazard (Chelsea), Neymar (Santos) y Andrea Pirlo (Juventus), Cristiano Ronaldo (R.Madrid) and Radamel Falcao (At. Madrid).

Messi is the current holder of the World Soccer award, which he also won in 2009. Only the Brazilian Ronaldo, with three, has more editions of the prize. Ronaldinho also won back-to-back World Soccer awards in 2004 and 2005. The winner will be selected by the readers of the British magazine.

Xavi, 150 international games with Barça

The Catalan midfielder is the first player in the Club’s history to play 150 international matches

Xavi has figured in 129 Champions League, 13 UEFA Cup, 5 World Club Cup and 3 European Super Cup games
 PHOTO: MIGUEL RUIZ-FCB

 Xavi Hernández continues breaking Club records and this Tuesday he became the first Barça player to play in 150 international games. He made his debut on the European stage on September 16th 1998 at Old Trafford and has now gone on to make 129 Champions League appearances, as well as 13 in the UEFA Cup, 3 in the European Super Cup and 5 in the World Club Cup. In those 150 games, he has scored 12 times – 10  in the Champions League and once in the UEFA and World Club Cups.

Xavi is followed by an illustrious list of Barça players, including Puyol, Víctor Valdés, Iniesta, Migueli, Messi, Guardiola, Sergi, Zubizarreta and Cocu and also figures in the top ten European players with most international appearances. Paolo Maldini leads that group with 181 games played, followed by Raúl González, Clarence Seedorf, Javier Zanetti and Ryan Giggs, legends of European football who Xavi is fast catching up on.

Seven titles

Those 150 games have seen Xavi win three Champions League titles (2005/2006, 2008/09 and 2010/11), two European Super Cups (2009/10 and 2011/12) and two World Club Cups (2009/10 and 2011/12). Seven international titles to add to the seven league titles, two Spanish Cups and five Spanish Super Cups which he possesses and which have made him an outstanding figure in the Club’s history, with 641 appearances in all competitions for the team he has dedicated his career to.

Champions League ranking 2012 - 2013 Round 1

Champions League ranking 2012 - 2013 Round 1

 TeamsTotalHomeAway
 Group APointsPWDLSGCG  PWDLSGCGPWDLSGCG
1Oporto6220030 110010110020
2PSG3210142 110041100101
3Dinamo de Kiev3210134 110020100114
4Dinamo de Zagreb0200204 100102100102
 Group BPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1Arsenal6220052110031110021
2Schalke 044211043101022110021
3Montpellier1201134100112101022
4Olympiakos0200225100112100113
 Group CPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1Málaga6220060110030110030
2Milan4211032101000110032
3Anderlecht1201103100103101000
4Zenit St. Petersburgo0200226100123100103
 Group DPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1Real Madrid6220073110032110041
2Borussia Dortmund4211021110010101011
3Manchester City1201134101011100123
4Ajax0200215100114100101
 Group EPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1Shakhtar Donetsk7321052220041101011
2Chelsea4311174101022210152
3Juventus3303044101011202033
4Nordsjælland1301217201115100102
 Group FPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1Valencia6320162110020210142
2Bate Borisov6320165210134110031
3Bayern Munich6320144110021210123
4Lille0300316200214100102
 Group GPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1FC Barcelona9330073220053110020
2Celtic4311144101000210144
3Spartak Moscou3310267210144100123
4Benfica1301214100102201112
 Group HPointsPWDLSGCGPWDLSGCGPWDLSGCG
1Manchester U.9330063220042110021
2CFR 1907 Cluj Napoca4311143100112211031
3Sporting Braga3310245100102210143
4Galatasaray1301214201113100101

Tuesday, October 23, 2012

Manchester, Chelsea bado wababe


IMG_0133

Liverpool yachipua, Arsenal waoga kichapo


Marejeo ya Ligi Kuu ya England (EPL) baada ya mapumziko yamekuja na wimbi la ushindi kwa baadhi ya vigogo wa ligi hiyo.
Licha ya kuanza kujifunga, Manchester United walifanikiwa kusawazisha makosa yao na kuwachapa Stoke City mabao 4-2.
Majirani zao wamwaga fedha, Manchester City, wakicheza watu 10 walifanikiwa kukwepa kipigo kwa West Bromwich Albion kwa kusawazisha na kushinda 2-1.
Vinara wa ligi hiyo, Chelsea waliendelea kutoa dozi, nao wakitoka kwenye mbinyo wa mabao 2-1 hadi kushinda kwa 4-2 nyumbani kwa Tottenham Hotspur na kujitanua kileleni mwa ligi.
Arsenal waliwashangaza wengi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 walipocheza nyumbani kwa Norwich City ambao tangu kuanza ligi hawajafanya vyema.
Lakini wana Anfield, Liverpool walikuwa na la kujivunia, baada ya kupata ushindi wa kwanza wa ligi nyumbani.
Lilikuwa bao la chipukizi Raheem Sterling anayeanza kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza, lililoondoa mkosi kwa Wekundu hao kwa kuwakandika Reading bao 1-0.
Wigan wameendelea na matatizo yao kwa kukandikwa mabao 2-1 na vijana wa Swansea waliokuwa wameanza kusinzia baada ya kuanza vyema msimu huu.
Ufufuko wa Southampton kwa upande mwingine, ulionekana kuwa geresha tu, pale walipokubali kisago cha mabao 4-1 kutoka kwa West Ham United ya Sam Allardyice.
Utata wa Aston Villa uliendelea, baada ya kuadhiriwa kwa kufungwa bao 1-0 na Fulham katika mzunguko huu wa nane wa EPL.
Edin Dzeko alikuwa shujaa wa mabingwa watetezi, Manchester City, kwani aliingia na kupachika mabao mawili katika dakika za mwisho mwisho na kuwanusuru City kupata kichapo cha kwanza cha ligi.
City walijikuta katika wakati mgumu baada ya James Milner kupata kadi nyekundu mapema, ikiwa ni ya kwanza tangu aanze kucheza soka, kutokana na rafu mbaya dhidi ya mshambuliaji wa West Brom,
Shane Long aliyekuwa anakwenda kufunga.
Wayne Rooney alijifunga mwenyewe kabla ya kuifungia Manchester United mabao mawili katika ushindi dhidi ya Stoke uwanjani Old Trafford.
Wengine waliofunga kwa United ni Robin Van Persie na Danny Welbeck.
Chelsea walibadili mchezo kwa mabao mawili ya haraka haraka ya Juan Mata yaliyofanya matokeo yasomeke 3-2 kabla ya Daniel Sturridge kuingia dakika za mwisho na kufunga bao la nne.
Andre Villas-Boas alitumia kila silaha aliyokuwa nayo kuwaadhibu mahasimu waliomfukuza kazi Machi mwaka jana.
Hata hivyo, alichopata ni mabao mawili tu kutoka kwa beki William Gallas na Jermain Defoe.
Kichapo cha Arsenal ni cha pili msimu huu, tena katika mechi tatu tu, safari hii ikiwa mikononi mwa Norwich ambao ni ushindi wa kwanza.
Ajabu ni kwamba Norwich walipachika bao dakika ya 19 tu ya mchezo kupitia kwa Grant Holt, na Gunners wakashindwa kulikomboa, licha ya kucheza kikosi kamili.
Kocha Brendan Rodgers wa Liverpool alikuwa katika bahari ya majaribu tena, kwani alikuwa akikabiliana na timu aliyoifundisha siku zilizopita.
Sterling anayechezea pia timu ya taifa alimng’arisha kwa kupachika bao kutokana na pasi nzuri ya mshambuliaji mwandamizi pekee aliyebaki kikosini, Luis Suarez.
Sterling anaweka historia ya kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi wa Liverpool baada ya Michael Owen. Sterling ana umri wa miaka 17 na ana asili ya Jamaica, japokuwa ameamua kuchezea timu ya taifa ya England.

Hakuna suluhu ubaguzi katika soka England..

IMG_0283



Wachezaji wamewatolea uvivu viongozi wao

Swansea, Wigan wagomea fulana za kampeni

Rio, Roberts, Pienaar, Cisse, Lescott vinara

Sakata la ubaguzi wa rangi kwenye soka limeingia hatua mpya, baada ya wachezaji kadhaa weusi kuwatolea uvivu wanafiki.
Mshambuliaji wa Reading, Jason Roberts, Mwingereza mwenye asili ya Grenada alivunja ukimya kwa kukataa kuvaa fulana inayoashiria upigaji vita ubaguzi huo.
Aliungwa mkono na wachezaji zaidi ya 30, akiwamo Rio Ferdinand wa Manchester United, wanaoamini kwamba taasisi ya Kick It Out haijachukua hatua stahili kuukabili ubaguzi. Imekuwa utamaduni kila Oktoba kuadhimishwa wiki ya kupinga ubaguzi, na wachezaji wote walitarajiwa kuvaa fulana hizo kwa wiki moja kuanzia Oktoba 18.
Matukio haya yamekuja baada ya John Terry wa Chelsea kumbagua Anton Ferdinand (mdogowe Rio anayechezea Queen Park Rangers – QPR) na Luis Suarez wa Liverpool kumtolea lugha ya aina hiyo Patrice Evra wa United, kisha kukataa kumpa mkono mara mbili.
wachezaji waliokataa kuvaa fulana hizo kabla ya mechi za mwisho wa wiki ni Victor Anichebe, Sylvain Distin na Steven Pienaar wa Everton waliokuwa wakipambana na QPR.
Wenyeji wao, yaani QPR waliokataa fulana hizo ni
Anton Ferdinand kama alivyotarajiwa, Djibril Cisse, Shaun Wright-Phillips, Nedum Onouha na Junior Hoilett.
Jumamosi wachezaji wengi zaidi waligombea fulana hizo, nao ni Micah Richards na Joleon Lescott wa Manchester City na Rio Ferdinand wa Manchester United.
Mwassi wa mgomo huo alitimiza azma yake katika uwanja wa Anfield, naye ni Jason Roberts wa Reading wakati Kenwyne Jones wa Stoke naye aliitupa mbali fulana hiyo.
Swansea na Wigan walionesha mshikamano wa ajabu kwani wachezaji wao wote hawakuvaa fulana hizo.
Hatua ya wachezaji hao kukacha fulana zenye nembo yenye maneno ya Kiingereza; ‘Mchezo Mmoja Jamii Moja’ imekuja baada ya Ashley Cole wa Chelsea pia kumtetea mshirika wake Terry kortini.
Cole ambaye ni mweusi aliku kubezwa na Chama cha Soka (FA) cha Uingereza kwa vile ushahidi wakeu ulikuwa wa uongo, naye akajibu kwa kuwatusi maofisa wa FA.
Matokeo ya hatua yake ya kiburi na majigambo imeishia kutozwa faini ya Pauni 90,000. Rio amemfananisha Cole na ‘choc ice’, yaani barafu ambayo nje huweza kuwa nyeupe na ndani nyeusi. Rio alipigwa faini ya Pauni 45,000.
Terry aliadhibiwa kulipa faini ya Pauni 220,000 na kukosa mechi nne za ligi, akadai angekata rufaa.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita amesema hatakata rufaa, hatua inayoonesha ameridhia adhabu zote na anajua kwamba alifanya makosa ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Anton.
FA ilimwadhibu Suarez kukosa mechi nane na kulipa faini ya Pauni 40,000 kwa makosa yake ya kujirudia rudia. Chelsea nao wamemwongezea Terry adhabu na walisema Cole naye angeadhibiwa, lakini Terry anabaki nahodha wa mabingwa hao wa Ulaya.
Wakati hatua hizo zikichukuliwa, taasisi ya Kick It Out inachukuliwa na wachezaji weusi kwamba imelemaa na haijakuwa makini kushughulikia tatizo hilo, hivyo wakaamua kuachana na fulana zao, ili walau kufikisha ujumbe.
Wakati makocha wa timu ambazo wachezaji wao waligomea fulana hizo wakionesha upole, Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson aligeuka mbogo, akidai Rio angeshughulikiwa.
Lakini ni Rio huyo huyo anayetegemewa na klabu yake katika ulinzi Jumanne hii katika hatua za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Jumatatu asubuhi, Rio na Ferguson walionekana mazoezini, wote wakitabasamu na kujenga hisia kwamba hapangekuwa na adhabu yoyote.
Yalichapishwa madai mwishoni mwa wiki, kwamba huenda Rio angeadhibiwa kwa kukatwa mshahara wa wiki mbili, ambao ni Pauni 220,000, na hatima yake Man U kuwa shakani. Si rahis kwa kocha Ferguson kuchukua hatua kama hiyo.
Hata angeadhibiwa Rio ni mtu wa msimamo na katika masahibu ya mdogo wake na mengine ya wanaodhalilishwa, amekuwa nao siku zote, bila kuogopa kitakachompata.
Pengine ni kwa sababu hiyo, Ferguson amekengeuka na kusema kwamba hakuna tatizo kati yake na Rio na kwamba mambo yote yameshawekwa sawa.
Akizunguza na waandishi wa habari Jumatatu alasiri, Ferguson alisema kwamba kilichotokea ni ukosefu wa mawasiliano kutoka kwa Rio, aliyetarajiwa kutoa notisi ya kusudio la kutovaa fulana hiyo.
Ferguson alionekana kuudhika, hasa kwa sababu alikuwa amemshambulia Roberts wa Reading kwa kutangaza kugomea uvaaji fulana, akisema kwamba mshambuliaji huyo hakuwa na hoja.
‘Kick Racism out of Football’ ilianza mwaka 1993 kabla haijabadilika na kuwa ‘Kick It Out’ mwaka 1997.
Katika msimu wa mwaka 2010/11 taasisi hiyo ilikuwa na bajeti ya £453,913. Kati ya hizo, £330,000 zilitolewa na FA, taasisi inayoendesha Ligi Kuu na Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA).
Akizungumzia suala la ubaguzi kwenye soka, Mark Hughes – Kocha Mkuu wa QPR anayochezea Anton Ferdinand anasema itachukua muda mrefu kumaliza tatizo hilo.
Kocha wa Everton, David Moyes anawaunga mkono wachezaji wake watatu kwa walilofanya, japokuwa anasema kwamba hiyo haina maana anakubaliana na hoja yao.
Ni vigumu kwa kocha yeyote mweledi kuwaadhibu wachezaji weusi kwa sababu eti wamekataa kuvaa fulana hizo, kwa sababu wapo wanaowatukana mara nyingi wasioadhibiwa. Itachukua muda kupata suluhu katika hili.

Tuesday, October 16, 2012

Safari ya Cole inafika mwisho Chelsea?

IMG_0147

Vidic naye adaiwa kuaga Manchester United


Beki wa kushoto aliyepata kudaiwa kuwa bora zaidi duniani, Ashley Cole anakaribia kuondoka Chelsea.
Mchezaji huyo aliyeichezea England mechi 98 tayari anawindwa na klabu tatu kubwa.
Mkataba wa Cole unaisha mwisho wa msimu huu, ambapo inadaiwa kwamba amepewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja tu asioutaka, kama ilivyokuwa kwa Didier Drogba.
Sera ya Chelsea imekuwa kwamba hakuna kutoa mkataba wa zaidi ya mwaka kwa wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 30, na Cole anayo 31.
Habari hizi zinakuja wakati beki huyo akiomba huruma ya Chama cha Soka (FA) England baada ya kuwatukana maofisa wake kwa kutumia mtandao jamii.
Cole alikasirishwa na jinsi FA kubeza utetezi wake kwa John Terry aliyemtusi kibaguzi Antony Ferdinand wa Queen Park Rangers (QPR). FA ilisema Cole ni mwongo na ushahidi wa Terry ulikuwa wa kutunga.
Wakati safari ya Cole ikikaribia ukingoni Stamford Bridge kama Drogba anayecheza China, makocha wake wa zamani, Jose Mournho wa Real Madrid na Carlo Ancelotti wa Paris Saint-Germain wanadaiwa kusubiri kumchukua.
Ni Ancelotti aliyetangaza hivi karibuni kwamba Cole ndiye beki bora zaidi wa kushoto, na kwamba klabu inayotaka uimara lazima imtafute.
Hata hivyo, si ajabu Cole asiondoke kwenye Ligi Kuu, kwani Kocha Mkuu wa Manchester United, Alex Ferguson anadaiwa kumtaka Cole siku nyingi.
Kama alivyomnyakua Robin Van Persie wa Arsenal mkataba wake ulipokaribia kumalizika Emirates, Ferguson anaelekea kunyatia mazingira ya Chelsea na Cole ili Januari aingie Old Trafford.
Lakini, kwa upande mwingine inadaiwa kwamba Cole anatikisa tu kiberiti wala hana mpango wa kuondoka, bali ni namna ya kupata mkataba mrefu au fedha nyingi zaidi Stamford Bridge.
Watu wa karibu naye wanasema kwamba Chelsea wanatakiwa kuonesha heshima kwa Cole kwa mchango aliotoa kwa timu hadi kutwaa kombe la Ulaya, kwani umri haujamzuia kucheza vyema.
Iwapo Cole ataamua kuondoka Chelsea kwa sababu zozote, kuna uwezekano wa nafasi yake kuchukuliwa na Benoît Assou-Ekotto wa Tottenham Hotspurs.
Taarifa zaidi kuhusu kuhama wachezaji zinamgusa nahodha wa Mashetani Wekundu, Nemnaja Vidic anayehusishwa na kuhamia klabu ya Kirusi inayomwaga noti, Anzhi Makhachkala, inayotaka kumpa mshahara wa Pauni milioni 12 kwa mwaka baada ya kodi.
Hata hivyo, si rahisi kwa Ferguson na United kwa ujumla kumwacha beki huyo wa Serbia aliyerejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu aondoke, kwani ni nguzo kubwa ya safu yao ya ulinzi.

Kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

13 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI TWFA

 normal_2Ofisi_Mpya_za_Shirikisho_La_Mpira_Wa_Miguu_Tanzania_TFF

Wagombea 13 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika juzi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, waliopitishwa kwenye nafasi ya uenyekiti ni Isabellah Huseein Kapera, Joan Ndaambuyo Minja na Lina Paul Kessy.
Makamu Mwenyekiti ni Rose Kisiwa wakati wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni Amina Ali Karuma na Cecilia Oreste Makafu. Mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Msaidizi, Macky Righton Mhango naye amepita kwenye usaili huo. Aliyepitishwa kwenye nafasi ya Mhazini ni Rose Stewart Msamila.
Furaha Francis na Zena Chande wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati waliopita kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia Ludovick Temba, Rahim Salum Maguza na Sophia James Charles.
Hivi mchakato wa uchaguzi wa TWFA uko katika kipindi cha kukata rufani ambapo ni kuanzia Oktoba 15-17 mwaka huu. Rufani zinatakiwa zifike kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Oktoba 17 mwaka huu.
Wagombea wawili ambao hawakupitishwa kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud walioomba ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF. Wagombea hao ambao pia walikuwa wamewekewa pingamizi hawakufika kwenye usaili.

PONGEZI KWA UONGOZI MPYA ARFA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 14 mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Pwani.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya COREFA chini ya uenyekiti wa Hassan Othman Hassan ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Pwani kwa kuzingatia katiba ya COREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Hassan Othman Hassan (Mwenyekiti), Riziki Majala (Katibu), Geofrey Irick Nyange (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Juma Haruna Kisoma (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Abubakar Allawi (Mhazini).
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika kisiwani Mafia ni  Musa Bakari Athumani, Godfrey Magnus Haule na Gwamaka Oden Mlagila. Mwakilishi wa Wanawake ni Florence Ambonisye.